Isaiah 10:24-27

24 aKwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni,
msiwaogope Waashuru,
wanaowapiga ninyi kwa fimbo
na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.

25 bBado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma,
na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.”


26 c Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi,
kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu,
naye atainua fimbo yake juu ya maji,
kama alivyofanya huko Misri.

27 dKatika siku hiyo mzigo wao utainuliwa kutoka mabegani mwenu,
na nira yao kutoka shingoni mwenu;
nira itavunjwa
kwa sababu ya kutiwa mafuta.

Copyright information for SwhKC